Nikki Mbishi Atangaza fursa kwa wasanii wa muziki.

Nikki Mbishi Atangaza fursa kwa wasanii wa muziki.

Nikki Mbishi ni moja kati ya watunzi bora wa nyakati zote katika muziki wa hiphop.

Na katika uhalisia ni moja ya wasanii ambao wana misimamo yao katika kusimamia kile ambacho anakiamini.

Kupitia mtandao wa picha ‘Instagram’ Nikki Mbishi ametangaza fursa kwa wasanii wa muziki ambapo ameandika ”
“Salaam,
Nikki Mbishi alias Unju Bin Unuq anapenda kuutaarifu umma wa Tasnia ya muziki kuwa kuanzia sasa atakuwa anawaandikia au kutunga mashairi ya aina zote za mahadhi ya muziki(GHOSTWRITING).

Kazi hizo zitafanyika kwa gharama nafuu zisizoumiza waganga njaa na hata wale waganga shibe yaani bei CHE.

Kwa wanaohitaji wafanye kucheck na namba hii 0786655677 au 0756837683.

Asanteni na nyote mnakaribishwa katika harakati ya kuimarisha tasnia zetu kwa uimara thabiti wa kimashairi.

#ZINGATIA
Kama sio biashara zichunie hizo namba maana hutopenda au kufurahishwa na “RIPLIES” zangu.
#Fursa #Fursani
#Unju @2018″

#TuzungumzeMuziki