Nikki Mbishi anapotoka kukataa mahojiano.

Nikki Mbishi anapotoka kukataa mahojiano.

Mara zote hunena yakuwa “Hakuna muziki usiokuwa biashara” isipokuwa “Biashara inahitaji matangazo nyakati zote”

Ndiyo maana tunaona kila leo makampuni makubwa ambayo tangu tumezaliwa yamekuwa yakiendelea vyema kujitangaza kwa upana tena kwa kutumia fedha nyingi.

Hiyo yote ni yakuwa “Biashara ni matangazo” lazima utangaze watu wajue vyema bidhaa yako.

Hivyo kitendo cha Nikki Mbishi kukataa mahojiano ni wazi anajiwekea mkwamo wa biashara yake ya muziki.

Mtandao pekee hamtoshi bali yapasa afanye mahojiano mengi ‘Media’ katika kutangaza vyema biashara yake.

Haipaswi hata mara moja kukataa mahojiano, kukataa mahojiano ni wazi anapotoka tena kwa upana wa hali ya juu.

Na inapaswa awe ni mtu wa mahojiano mengi kadri awezavyo ili kuitangaza bidhaa yake ya muziki.

Na mswahili hunena yakuwa “Kiburi si muungwana, muungwana ni kitendo” Na akumbuke biashara ni mahusiano, kwa maana hivyo kitendo cha kuwakatilia watu mahojiano ni wazi inaharibu mahusiano yake na watu hao.

Kimsingi si jambo jema, Nikki anapaswa kutafakari kwa upana, hisia zenye hasira hazipaswi kumuendesha vyema.

Uwezo wake na ubora wa kipaji chake ni mkubwa mno, lakini kama hakuna matangazo ya biashara na mahusiano hatoenea kwa ukubwa.
#TuzungumzeMuziki