Nikki Mbishi Amuhoji Diamond Platnumz juu ya uuzaji wa nyimbo.

Nikki Mbishi ni miongoni mwa wasanii wa hiphop ambao wamekuwa wakiheshimika zaidi katika mitaa na vijiwe vya hiphop hapa nchini Tanzania lakini hata nje ya nchi.

Pumzika mwili wako ni wimbo wake mpya unaokuja hivi karibuni, ambao tayari ameshaanza kuweka vionjo na mashairi ya wimbo huo katika kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii.

Mapema leo kupitia mtandao wa twitter Nikki Mbishi amemuuliza swali msanii Diamond Platnumz ambapo Nikki ameandika “Samahani bwana hivi kule ni kila msanii anaweza kuji-register kuuza kazi zake au ni watu fulani? Nikki hakuishia hapo ambapo aliandika tena “Maana hata zile namba mlizoweka kwenye site moja haipo,nyingine inaita haipokelewi na sasa haipatikani kabisa. Cc

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa

Mwisho.