NI WAZI NIKKI WA PILI AMEJIKANYAGA

IMG_6227

Picha hii ilipigwa tarehe 4/2/2016 siku ya alhamis wakati akaijaza form za kujiunga na Tuma maneo ya Basata.

NI WAZI NIKKI WA PILI AMEJIKANYAGA

Kuuliza ni njia moja wapo ya kujifunza na kupata ufahamu juu ya jambo Fulani.Wenye busara mara zote huuliza ili waweze kupata kujua zaidi juu ya kitu asichojua.

Ni wiki kadhaa zimepita tangu andiko la kikao cha wasanii sehemu ya III kutoka na kupata maoni ya watu walio wengi. Wapo waliosema vibaya wapo walisema vizuri lakini mwisho wa siku yote ni maoni.

Kupitia mtandao wa Twitter msanii chipukizi Nikki wa pili alitoa maoni yake, hii haikatazwi hata mara moja mtu kutoa maoni katika jambo lolote lenye kujenga au kubomoa. “siwezi kujifunza kwa wajinga” hii ni moja kati ya yale mengi aliyoandika kuhusu tizneez katika ukurasa wake wa Twitter.

Kuna kitu watu wengi hawajui na mara nyingi wamekuwa wakijichanganya/ wakijikanyaga katika mambo haya, Elimu na Ufahamu. Kuna tofauti kubwa kati ya elimu na ufahamu, unaweza kuwa na elimu lakini ukakosa ufahamu na unaweza ukakosa elimu na ukawa na ufahamu.

Mgema akisifiwa tembo hulitia majiNaamini katika msemo huu, wapo watangazaji, wadau na hata mashabiki wanaomsifia msanii chipukizi Nikki wa pili katika mambo mengi, hasa uchambuzi wa mambo yanayojenga jamii.

Ni wiki kadhaa tu zimepita tangu tizneez iandike kuhusu TUMA ambacho ndicho chama cha muziki wa kizazi kipya. Katika andiko hilo lilieleza Tuma ina wanachama wangapi na hata umuhimu wa msanii wa kizazi kipya kujiunga au kuwa ndani ya chama. Na tizneez iliandika kuhusu TUMA kwasababu ni blog inayoandika kuhusu Bongo fleva/hiphop yani muziki wa kizazi kipya.

Msanii chipukizi Nikki wa pilI kupitia twitter aliandika “Tuma kwa miaka mingi haijawahi kuwa hata na wanachama hai 50??? Hawa 250??? Umewatolea wapi.ndugu mwandishi?

Ni wazi hapa ulijikanyaga maana wakati unaandika haya hukuwa mwanachama wa TUMA je haya uliyajuaje? Ni wazi alipata majibu mazuri kutoka kwa Katibu wa TUMA siku ya kikao kilichofanyika Basata tarehe 4 mwezi huu ambapo tena aliuliza kuwa TUMA ina wanachama wangapi na Katibu akamjibu 250.

“Ujinga ni kukisifia chama ambacho wasanii wenyewe hawa mjui mwnyekiti hata kwa sura” Ni wazi tulisifia TUMA maana tulipata ufafanuzi juu ya mambo yanayofanywa na TUMA, hakika ni mengi mazuri hivyo ni lazima mtu mwenye ufahamu usifie. Mwenyekiti wa Tuma ni ndugu Fredrick Malick ambaye ni maarufu kwa jina la Mkoloni ambaye ndiye msanii anayeunda kundi la Wagosi wa kaya. Je ni kweli wasanii hawamfahamu kwa sura Mgosi Mkoloni?

ujinga ni kuhoji uanachama kwenye chama ambacho hakina hata ofisi” haikuwa kosa kuhoji unachama wake TUMA maana ni msanii chipukizi anayefanya vizuri hivyo ni vyema kujiunga na chama ili kusimamia mengi yaliyo mazuri. Napata mashaka kusema chama hakina ofisi nadhani kauli yake ya kusema “siwezi kujifunza kwa wajinga” inazidi kunipa wasiwasi ni kitu gani alikuwa anamaanisha sitaki kuamini kama amekuwa mjinga wa kiwango cha juu kusema chama hakina ofisi na huku ameomba kuwa mwanachama wa TUMA.

uhalali unaanza kwa chama kwenda kwa wanachama sio kwa wanachama kwenda kwa chama…mgombe humfuata mwananchi bro” Kuna haja ya kuendelea kupeana elimu juu ya mambo yenye msingi. Ni wazi chama cha muziki wasanii wanapaswa wakijue na wakifuate maana kinatetea haki zao. Ila kuna mengi yamejificha nyuma kabla ya Tuma wapo waliowahi kuanzisha hata kampuni na wasanii wengi waliifuata kujua ndicho chama chao na baada kuona haikuwa sawa na wengine kurudi kujiunga na TUMA hii ni kwa mujibu wa Mkoloni. Je kitendo cha kuja Basata tarehe 4/1/2016 ni kweli chama kimlikufuata?

Nyakati zinaenda na hata siku ya alhamis ya tarehe 4/1/2016 msanii Nikki wa pili alipokelewa na kuwa mwanachama wa TUMA. Lakini imekuaje mpaka amejiunga kwenye chama kisicho na ofisi, chama ambacho mwenyekiti wake hajulikani hata kwa sura, chama ambacho hakina hata wanachama 50 hii ni kwa mujibu wa Msanii Chipukiz Nikki wa pili.

Wapo wenye hisia tofauti kwa msanii huyu kujiunga kwenye chama hicho,lakini tusiandike sana kuhusu hisia zetu tusubiri muda utasema

Unaweza kusoma tweet zake chini hapo

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez

tweet 7 tuma

maklaaa 3

makalaaaa 2

makalaa 5

Mwisho/itaendelea