Ni ngumu kurudi kufanya kazi na Tiptop Connection- Cassim Mganga

Ni ngumu kurudi na kufanya kazi na Tiptop Connection- Cassim Mganga

Haiwezekani ni wimbo ambao ulimtambulisha vyema Cassim Mganga kwenye ramani ya muziki wa kizazi kipya.

Tiptop Connection ni moja kati ya makundi makubwa ambayo yamewahi kuwa na wasanii wengi wa kwa wakati mmoja. Ambapo kundi hilo lilikuwa likiundwa na wakali kama Z Anto, Keisha, Pingu, Denso, Spark, Cassim, Tunda Man, Dogo janja, Madee, Pnc, na wengine wengi.

Cassim alikuwa ni miongoni mwa wasanii ambao waliojitoa katika familia hiyo miaka kadhaa nyuma. Mapema wiki tumeaona akishare picha yenye nembo ya Tiptop Connection, Team Tizneez haikusita kumtafuta ambapo Cassim alitoa ufafanuzi juu ya posti yake hiyo.

Cassim amesema “Kwani kuna maneno ambayo yana ashiria kurudi TipTop? Kwaiyo nikipost neno la Tiptop maana yake nimerudi TipTop? nitaendelea kuiwakilisha Tiptop maana ni familia yangu na popote nitakapo kwenda TipTop ni ya kwangu. Ila kurudi na kufanya kazi  kama zamani nilivyokuwa nina mikataba ilo ni ngumu maana nina watu wangu nyuma pia nina mipango yangu ila kuna watu pia nataka kuwainua.

Hivyo ni watu kama familia na tunaweza kufanya lolote kama familia ila kwa mikataba ya kikazi hilo hamna.”

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube Tizneez