NEY WA MITEGO AWAFUNGIKIA WASANII WENZAKE

IMG_2511

Siku 30 kuelekea uchaguzi mkuu wa Tanzania ndio siku pekee zilizobaki, Wakati kampeni zikiwa zinaendelea na wasanii wengi kuonekana wapo katika pande tofauti katika vyama na kupelekea kutumia zaidi kurasa zao za mitandao ya kijamii katika kutetea kiongozi anayemkubali pia kutoa maneno ya dhihaka kwa kiongozi mwingine.

Msanii Ney wa mitego hakusita kuweka hisia zake katika mtandao wa picha instagram  ambapo aliaandika”

Wasanii tubaki kua wahamasishaji tu!Kuanza kukashfu Viongozi utadhani labda nawewe umekua mwana Siasa au Mgombea itakuja kutu Cost baadae. Hua najiuliza cjui wanalipwa shiling ngapi maana wanasahau wao ni wasanii na wana Mashabiki wenye Imani tofauti, pia kuna Maisha baada ya uchaguzi. Endeleeni kutumika vibaya kwa Njaa ya leo na kwa maslahi ya wachache na kusahau kuna kesho. Pigania unacho amini but si kwa kashfa wala Matusi. Mimi naamini ‪#‎Mabadiliko2015‬ .Tukutane ‪#‎October25‬

Unaweza kuwa rafiki yetu

facebook.com/tizniz

instagram.com/tizneez

twitter.com/tizneez