Ndivyo inavyopaswa kwa Vanessa Mdee na Jux katika nyakati hizi

Ndivyo inavyopaswa kwa Vanessa Mdee na Jux katika nyakati hizi.

Waswahili hunena “Tumia nyakati kwa nyakati, maana nyakati hupita na hazirudi”

Kwa hakika ni nyakati nzuri katika kujiongeza na kuweza kupita katika maeneo mengi juu ya tamasha lao la muziki ambalo lina ubatizo wa jina la “ILAM” (In love and money)

Na jambo jema ni kuwa kila tumbuizo litakuwa laonekana kupitia kituo cha runinga Clouds Plus.

Licha ya Jux na Vanessa kuwa wahusika wakuu lakini wasanii toka Mdee Music watakuwepo, lakini G nako ni miongoni mwa wasanii ambao wametajwa mapema kuwa watakuwepo.

Tukisema muziki umekuwa ni katika muendeno huu wa wasanii kuweza kufanya safari zao za matamasha yao binafsi ya muziki, na sio kusubiri promota akuite mahala husika.

Sisi tunaamini katika ILAM na kuona pia itazidi kufungua mwanga kwa wasanii wengine wengi.

#TuzungumzeMuziki