Ncha Kali ampendekeza One The Incredible na Brian Simba kwenye marudio ya wimbo wa Ray Vanny

Ncha Kali ampendekeza One The Incredible na Brian Simba kwenye marudio ya wimbo wa Ray Vanny

Wakati Pochi Nene wimbo wa Ray Vanny ukiendelea kufanya vyema katika uwanja wa muziki wa kizazi kipya, tayari msanii Ray Vanny ameshaanza kuweka video fupi kwenye mtandao wa picha ‘Instagram’ na wasanii wengine katika marudio ya wimbo huo.

Na mpaka sasa wasanii ambao tayari wameshajulikana kama wapo katika marudio ya wimbo huo ni Kaligraph Jones tokea Kenya, lakini Country Boy wa hapa nyumbani Tanzania.

Na kupitia mtandao wa picha ‘Instagram’ katika posti ya Ray Vanny ya usiku wa kuamkia leo, Ray Vanny aliuliza nani mwingine unataka kumsikia?

Na mtangazaji wa zamani lakini sasa mdau na mshauri wa sanaa ya muziki wa kizazi kipya Ncha Kali amependekeza wasanii wawili.

Ambapo wasanii hao ni One The Incredible na Brian Simba.

Je! wewe shabiki unadhani ni msanii gani mwingine anafaa katika marudio ya wimbo huo?

Tuambia hapa chini #TuzungumzeMuziki