NASH MC AWAHUSIA WATANZANIA

nash
Moja kati wasanii wa hip hop kutoka maeneo ya Temeke Dar es Salaam ,ambaye amejijengea umaarufu mkubwa kwa kuwa na misimamo mbalimbali zaidi katika muziki wa hip hop.Nash Mc aliyewahi kufanya vizuri na nyimbo kama,Zima, Tabia, Kaka Suma, Nazinduka pamoja na nyingine nyingi.
Nash Mc kupitia ukurasa wake wa Facebook amewahusia kwa kusema “Kaka na dada zangu watanzania nawaomba tuwe makini sana,kuna mipango inafanywa ya kutogombanisha watanzania kupitia dini hasa Waislamu na Wakristo kuna baadhi ya matukio ni wazi kabisa yanapangwa na watu au mataifa ya nje kwa maslahi yao binafsi, tumeishi miaka mingi pamoja bila matatizo ya aina yoyote kwa muda mrefu, tunashirikiana kwa mambo mengi tu lakini inaonekana wazi wapo baadhi ya watu au mataifa yanayopanga haya mambo. Mfano tumeuona kwa wenzetu wa nchi ya Afrika ya kati jinsi walivyoingia kwenye vita ya kidini na kusababisha maafa na vifo vya maelfu ya watu.Mwenyezi Mungu Tunusuru.”
Mwisho.