Nash Mc Asifu uwezo wa Fanani

maxresdefault

Fanani si jina geni kwa wapenzi wa muziki wa bongo hiphop, Fanani ni moja kati ya wasanii waliokuwa wanaunda kundi la Hard Blasterz ambalo ni wazi ni moja kati ya makundi yaliyochangia kukua na kueneza Bongo fleva.

Nash Mc katika muendelezo wa kutengeneza kanda mseto yake ambayo bado hajaipa jina wala kusema ni wimbo upi utatangulia kwenye vituo vya radio na runinga, ameonekana akiwa studio na mkongwe Fanani ambapo ni wazi amemshrikisha katika wimbo mmoja wapo.

Akiongea na Team Ladha 3600 Nash Mc alisema “Kiukweli nimefanya kazi na Fanani, kiuhalisia ni msanii ambaye namkubali zaidi. Hakika ni msanii ambaye anajua jinsi gani ya kucheza na maneno ya kiswahili, na kama unavyojua mimi ni mmoja wa watu ambao tunapigania sana matumizi ya lugha ya kiswahili. Jamaa ana uwezo jamaa ana kipaji cha hali ya juu. Ni wazi uwezo wake si wa kubahatisha na hata katika wimbo wangu Hasi 15 nimemtaja “Namkubali Fanani pale HBC”

Watu wakae mkao mzuri Nash Mc nimekuja tena na kanda mseto hii na nyimbo nyingi”