Nash Mc Ajibu hoja za Prof Jay asema “Upumbavu Ni kipaji cha mtu haijalishi umri”

Nash Mc Ajibu hoja za Prof Jay asema “Upumbavu Ni kipaji cha mtu haijalishi umri”

Baada ya Mkongwe wa muziki wa hiphop Tanzania Prof Jay ambaye kwasasa ni Mh Mbunge wa Jimbo la Mikumi liliopo mkoani Morogoro kupitia tiketi ya Chadema chini ya mwamvuli wa ukawa, mara baada kuandika mitazamo yake juu ya wasanii wa hiphop Tanzania. Ambapo mitazamo yake imegumsa zaidi msanii wa hiphop Nash mc.

Kupitia mtandao wa Twitter nae msanii Nash Mc hakuweza kukaa kimya juu ya mitazamo ya Prof Jay ambapo ameandika ”Sijui utaenda nchi gani ukute hakuna Hip Hop. Hip Hop aihitaji Kuvuka boda. Ivuke boda iende wapi? Mbinguni?“

“Nina uhuru wa Kuongea nachotaka almuhimu nisivunje sheria za nchi,hakuna pimbi yoyote anaweza kunipangia swali la kuuliza kwenye muziki.”

“Upumbavu Ni kipaji cha mtu haijalishi umri.”

“Nidhamu ya uoga kwangu ilikaaga upande wa kushoto kitaaaaambo.” Nash Mc alimaliza kwa kwa kuandika “Mtu mwenye nidhamu ya uoga akiambiwa jambo huona anachukiwa.”

 

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa