NASH MC “AFURAHISHWA NA KAZI ZAKE KUKUBALIKA SOUTH AFRICA

index
Nash Mc Rapper kutoka Temeke ambaye ni moja kati ya wasanii wa hiphop wenye misimamo mikali katika muziki huo.Nash amewahi kufanya poa na ngoma kama,Zima,Naandika,Asuyehusika na hiphop,Hasi na nyingine nyingi.
Nash Mc ambaye sasa yupo South Africa amesema”Ni Kama siku 5 nilikuwa Kimya na ukimya huo ulikuwa umesababishwa na Safari yangu ndefu ya kuelekea nchini Afrika Kusini,na niliingia huku siku ya Jumanne yani juzi.Namshukuru sana Mungu kwa kunijaalia Safari yangu kuwa ya salama na Amani. Na pia nawashukuru sana watanzania wenzangu ambao wanaishi Hapa Johanersburg kwa kunipokea vizuri,kikubwa nilichofurahia ni kuona kazi zangu zinakubalika sana katika masikio ya watanzania waishio Hapa,Pretoria,Jozi mpaka Cape Town. Kwa sasa nimewapa taarifa hii fupi tu lakini mipango zaidi ya show inafanywa na taarifa zitatolewa pale mambo yatakapokuwa tayari.
Sitachoka kupambana na kuwa mfano kwa wengine mafaniko hayawezi kuja bila kuthubutu.

Nash dizonga
Nash kwa Mandela
Nash Jozi
Nash Pretoria
Nash Cape Town