NANI ALAUMIWE KATI DOGO JANJA,MADEE NA BABU TALE?

madee

NANI ALAUMIWE KATI DOGO JANJA,MADEE NA BABU TALE?

Ni wiki 7 kama sio 8 tangu kutoka kwa wimbo wa My life wa mkali Dogo Janja ambaye yuko chini ya Tiptop Connection. Hakika alikata/amekata kiu ya mashabiki hata wapenzi wa muziki wa kizazi kipya katika ujio wake wa My life.

Ni baada tu ya kutoka wimbo wake wa My life Team tizneez ilimpa andiko la (Dogo Janja Anastahili Pongezi) kumsifu katika ujio wake huu , ambapo alikaa kimya kwa miaka 3 bila kutoa wimbo wowote. Hivyo haikuwa kazi rahisi kurudi kwa jinsi ambavyo alirudi, maana muziki wa sasa una ushindani mkubwa.

Mapema leo kumekuwepo na sintofahamu juu ya wimbo huu wa My life. Ikumbukwe wakati Dogo Janja kitambulisha wimbo katika kituo kimoja cha Radio ambapo aliambata na Babu Tale pamoja Madee, Dogo Janja alisema “Producer wa wimbo huu ni Carl Hovind kutoka Norway, na wimbo huu nilitakiwa nikarekodi huko nchini Norway, ila hati yangu ya kusafiria ilisumbua hivyo ikabidi atume mdundo ili niweze kufanya hapa hapa”.

Hatere ni wimbo wa Admiral P Feat Onklp ambao una mfanano na wimbo wa Dogo janja wa My life. Wimbo huu wa Admiral P ulitoka mwaka 2014 na ulikuwa unapatikana katika album ya Selvtillit &tro.

Team tizneez ilizungumza na Dogo Janja juu ya wimbo huu wa Hatere,akiongea kwa njia ya simu alisema “Mimi sikuwa nafahamu kama mdundo huu uliwahi kutumiwa, lakini pia hii ni Ridim mtu yoyote anaweza kufanya. Lakini pia kule kwa wenzetu ni kawaida maana mdundo ni mali ya mtayarishaji, ila pia mtayarishaji huyu atakuja hapa Tanzania hivi karibuni hivyo ni vyema tukasubiri.”

Maneno yamekuwa mengi hasa kwa wapenzi wa muziki wa kizazi kipya, wapo wanaomlaumu Madee na Babu Tale kwamba kwanini hawakusema kama huo mdundo uliwahi kutumika hivyo Dogo Janja ametumia kama Ridim tu. Maana isingeleta mtazamo hasi, au walifikiri si rahisi watu kufahamu wimbo huo?

Licha ya mdundo, lakini pia melody zimekuwa na mfanano zaidi kitu ambacho kinaendelea kuwapa hisia hasi wapenda muziki.

Usikilize hapa wimbo huo wa Hatere wa Admiral P Feat Onklp

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez