Nandy azindua bidhaa ya mafuta ya kupaka na sabuni ya kuogea.

Nandy azindua bidhaa ya mafuta ya kupaka na sabuni ya kuogea.

Ninogeshe ni wimbo wake ambao unafanya vyema kwenye uwanja wa muziki wa kizazi kipya, ambapo kwasasa Nandy ni moja ya wasanii wakike wenye ushawishi zaidi kwenye muziki.

Mapema leo Nandy ameweza kuzindua bidhaa zake za mafuta ya kupaka na sabuni ya kuogea kwa kushitrikiana na kampuni ya Grace Product Limited.

Nandy anaingia katika kundi la wasanii ambao wamewekeza nje ya muziki, ambapo ni wiki moja nyuma tuliandika andiko ambalo tumesema “Kuweza nje ya muziki kwa msanii iwe ni jambo la lazima”.

Tizneez tunampongeza Nandy kwa hatua hii kubwa ya uwekezaji wa nje ya muziki wake.

 

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa