Nandy aomba radhi kwa famalia yake, mashabiki na Serikali

Nandy aomba radhi kwa famalia yake, mashabiki na Serikali.

Kupitia mtandao wa picha ‘Instagram’ msanii wa muziki wa kizazi Nandy ameomba msamaha juu ya video yake ya faragha akiwa na msanii mwenzake Billnass.

Kupitia mtandao huo ameandika “Napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba radhi SANA SANA familia yangu, Ndugu zangu, Mashabiki wangu na Serikali kwa kilochotokea …Bado siko sawa.. naomba mniombee uzima 🙏🏽”

Sisi ni nani hata tusisema yakuwa anapaswa kusamehewa maana amejua kama amekosa, lakini nyakati zote hujifunza kutokana na makosa.

Hivyo nasi tupo katika kundi la wenye kujua thamani ya neno radhi,na kusema ni vyema tuzungumze muziki wake.

Mswahili hunena yakuwa “Ni ya kheri akubaliye kosa, maana amepata funzo ilihali faraja”

#TuzungumzeMuziki.