NAHREEL “NINA BAHATI KUMPATA AIKA”

navy-kenzo-2

Nahreel ndiye mtayarishaji bora kwa mwaka 2014-2015 kwa mujibu wa tuzo za KTMA. Nahreel ambaye kwa sasa ni mtayarishaji katika studio za Industry ambazo pia ndio studio zinazosimamia kundi lake la Navy Kenzo ambalo kwa sasa linafanya vizuri na wimbo wake wa Kamatia.

Nahreel na Aika ni wasanii wanaounda kundi la Navy Kenzo ambao wana mahusiano ya kimapenzi.

Nahreel hakusita kuweka wazi hisia na ukweli wake juu  ya Aika ambaye ni mpenzi wake wanaofanya pamoja shughuli zao za muziki.

Nahreel alisema “Namshukuru mungu ameniletea mtu sahihi kwangu, najiona mwenye bahati. Shida na raha tulizopita lakini bado tupo pamoja kiukweli namshukuru Mungu.”  Pia aika nae kwa upande wake alisema “hata nikisema nitasema hayo hayo tu”

Picha chini Nahreel na AIka wakiwa pamoja katika picha.

navy-kenzo

www.tizneez.com

Twitter tizneez
Facebook tizneez
Instagram tizneez

Youtube tizneez

 

Source Pillow Talk Times Fm