Nahreel ndiye aliyeandaa wimbo wa kombe la Dunia 2018.

Nahreel ni moja ya wasanii ambao wanaunda kundi la Navykenzo akiwa na msanii mwenzake Aika ambaye pia ni mzazi mwenzake.

Nahreel pia ni moja kati ya watayarishaji wazuri katika muziki wa kizazi kipya. Mapema kupitia mtandao wa Picha ‘Instagram’ Nahreel ameandika “Pleasure to produce the World Cup 2018 Anthem song featuring #JasonDerulo and @diamondplatnumz song called #Colors available now in all platforms #Cocacola

Hakika ni jambo jema na zuri katika hatua ya uandaji wa wimbo huu kwa upande wa Nahreel lakini muziki kwa ujumla kwa upande wa watayarishaji wa muziki.

#TuzungumzeMuziki

Attachment