NAHREEL “NASHANGAZWA NA WADADA WA SIKU HIZI”

index
Mtayarishaji bora wa muziki 2015-2016 kwa mujibu wa tuzo za Kill Music Awards zinazotolewa kila mwaka hapa nchini Tanzania.Hata hivyo Nahreel ni muimbaji na mwanzilishi wa kundi la NavyKenzo akiwa pamoja na mkali Aika.
Katika kipindi cha Mkasi kinachorushwa na Eatv chini ya mtangazaji machachari Salama Jabir,Nahreel alisema”Siku hizi nashangazwa na wadada walio wengi,unajua wadada wengi wa sasa hawana ndoto.Wanapenda zaidi mambo ya haraka haraka.Zamani wadada walikuwa na ndoto mfano zamani mtu anasema nataka niwe daktari au nataka kuwa fulani kitu ambacho hakipo sasa kwao.”
Nahreel pia alisema kwenye suala lake la studio anaweza akampa msanii beat na kama hajaifanyia vizuri akamnyanganya na kumpa msanii mwingine.si kwa lengo baya ila kama unashindwa kutendea haki mdundo ni wajibu wangu kumpa mwingine.”alisema

Twitter @tizneez
instagram @tizneez
facebook.com/tizniz