MZUNGU KICHAA AVUNJIWA KIOO CHA GARI NA KUIBIWA

Mzungu_Kichaa

Mzungu kichaa ni msanii anaefanya Bongo fleva mwenye asili ya Denmark lakini amekua hapa nchini Tanzania.Mzungu kichaa amewahi kufanya vizuri na ngoma zake kama,jitolee,Oya oya,wajanja,ujumbe na nyingine nyingi.

Kupitia mtandao wa facebook Mzungu kichaa ameandika “Leo nimevunjiwa kioo kwenye gari wakati nipo kwenye mahojiano. Wameondoka na laptop aina ya MacBook Pro yenye cover nyeusi. Niko tayari kutoa hela ndefu kwa mtu yeyote atakaeweza kunisaidia kuipata tena. Maana ina kazi zangu mpya za mziki nyingi. Niliibiwa Mikocheni karibu na eatv. Please share this post. Naomba msada wako. Dah. Nimeumia sana.”

Kama umeguswa na unajua inaweza kupatikana wapi basi unaweza kuwasiliana na mzungu kichaa au hata kwenye media yoyote ile ili aweze kupata mali yake.

Twitter@tizneez

instagram@tizneez

facebook@tizneez