MWANA FA, DITTO,NA NIKKI WA PILI WAJIUNGA TUMA

IMG_6227

Tanzania Urban Music Association (TUMA) ambacho ndiyo chama cha muziki wa kizazi kipya,TUMA haikusita kuweka wazi madhumuni yake ambayo ni Kuwaunganisha wasanii wote chini ya chombo kimoja chenye jukumu moja la kueneza na kukuza sanaa nchini kwa kuwaendeleza wasanii wa kizazi kipya. Kujenga uhusiano wa kindugu baina ya wasanii wa kizazi kipya ndani na nje ya Tanzania . Kuimarisha wajibu wa wasanii wa kizazi kipya wa kueleza, kueneza na kukuza, kwa kuitangaza nchi kwa njia ya sanaa. Kuwa kiungo na kutoa ushauri kwa wasanii wa kizazi kipya kuhusu maendeleo na matatizo ya sanaa nchini Tanzania. Kusimamia na kutetea haki miliki za wasanii wa kizazi kipya kwa kushirikiana na vyombo husika . Kitapokea na kusimamia misaada, ruzuku na michango kutoka kwa wafadhili iliyotolewa kwa ajili ya chama. 7. Kuwa chombo cha kutatua matatizo ya wasanii wa musiki wa kizazi kipya nchini. Kusaidia uwezekano wa upatikanaji wa mikopo ya biashara ya muziki kwa wasanii. Kuwaweka wasanii katika chombo kimoja ambacho kitakuwa na sauti kwa niaba ya wasanii wote wa nchini Tanzania. Kusisitiza serikali kutengeneza mazingira mazuri ya sanaa ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania katika kutetea na kupata maslahi yao.
Mapema leo katika kumbi za Basata Ilala Dar es salaam ambapo kulifanyika kikao hicho, ambacho madhumuni yake yalikuwa manne tu.
Moja ya madhumuni ilikuwa ni Kujiandaa na uchaguzi wa shirikisho, Kupanga tarehe na kugawa form za uchaguziwa Chama, Taarifa za utendaji wa chama na hata kupokea wanachama wapya.
Katika kupokea wanachama leo wasanii watatu wamepokelewa na Katibu ndugu Brayton ambaye alikaiumu nafasi ya Mwenyekiti, Ndugu fredrick Marick
Wasanii wapya waliopokelewa katika chama hicho ni Nikki wa pili,Mwana Fa na Lameck Ditto.Licha ya msanii Cyril kuchukua form za kujiunga.
Hata hivyo muitikio wa wasanii katika mkutano huo ulikuwa ni wa chini zaidi,ambapo ni wasanii 7 tu ndio waliojitokeza.
Picha za kikao hicho hizi hapa chini
IMG_6243

Baada ya kikao wasanii walipata picha ya pamoja

IMG_6227

wasanii wakiwa katika kikao hicho mazungumzo yakiendelea

IMG_6229

wasanii katika mazungumzo

IMG_6234

Picha juu katibu wa Tuma ambaye ndiye aliyekaimu nafasi ya mwenyekiti akiongea jambo

IMG_6241

Msanii Nikk akiandika mambo kadhaa wakati wa kikao

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez