“Muziki wa bongo fleva/hiphop hauna usawa”

“Muziki wa bongo fleva/hiphop hauna usawa”

Nimezungumza na Ferooz takribani dakika 5, moja ya swali ambalo nilimuuliza anadhani ni kwanini hafanyi vizuri kwenye huu muziki mwepesi wa bongo fleva sasa?

Hakusita kuweka wazi ambapo amesema “Kwenye muziki sasa hakuna usawa wa muda wa hewani, mtangazaji anataka umpoze anataka hela. Sawa sisi tunafanya game tunajua, msanii wa sasa analipiwa package ya air time kubwa hivyo ni ngumu kwa msanii wa zamani anajua ngoma ikiwa kali itaenda tu.

Watangazaji watazame muziki wanaupeleka wapi, kwasababu wakiangalia maslahi muziki unakufa. Maana msanii atajua nikifanya wimbo wowote cha muhimu video kali naenda pale natoa hela  basi nitashine lakini sio kusema wimbo ni mzuri. Kwaiyo unavyoona muziki unaelekea pabaya sababu tunaangalia ni pesa zaidi sio jamii inaenda wapi.”

Lakini kuweka mambo wazi ndio kumaliza tatizo, ambapo ingekuwa ni jambo jema na zuri kuwataja watangazaji na Madj wapenda pesa (Rushwa) ili tuweze kukomesha tatizo hili.

Ferooz amesema “Mimi siwezi kumtaja mtu siwezi kuongea live siwezi kumtaja mtu Fulani lakini ni kitu ambacho kipo wazi na wasanii wanaelewa. Sasa hizi wasanii hawaendi na sanaa wanaenda na Rushwa. Mimi sitaki beef na watu ila ambao wanakwamisha game wanajijua”

Rushwa imechukua nafasi kubwa katika muziki sasa, lakini kama wasanii wataamua kuwataja watangazaji hao na madj wao hakika tatizo litakwisha. Lakini kama wataendelea kukaa kimya na kulalamika pembeni basi lazima swala hili litakuwa na nalitawanufaisha watangazaji ilihali hao wameajiliwa na kulipwa mishahara na kampuni husika

“Amka msanii muda ndio huu”

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube Tizneez