Mtazamo wa Nikki Mbishi juu ya wasanii watuhumiwa wa madawa ya kulevya.

Mtazamo wa Nikki Mbishi juu ya wasanii watuhumiwa wa madawa ya kulevya.

Play Boy ni wimbo ulioweza kumfanya apate umaarufu mkubwa katika ramani ya muziki wa hiphop hapa nchi Tanzania.

Lakini pia Nikki Mbishi amewahi kufanya vyema na wimbo kama, Nyakati za mashaka, Dakika mbili Kill yourself, AKA, Tulikuwepo na nyingine nyingi.

Kupitia sakata ambalo linaendelea sasa juu ya Mh Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Paul Makonda kutaja list ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya bongo muvi na hata watu wengine maarufu juu ya kujihusisha na madawa ya kulevya kwa namna mbalimbali.

Nikki Mbishi hakusita kuweka mtazamo wake kupitia mtandao wa ‘twitter’ambapo ameandika ‘Siku washukiwa wa tuhuma za madawa ya kulevya hususani wasanii wakiwajibishwa kwa mujibu wa sheria nitaamini Serikali ipo.

Lakini pia Nikki Mbishi aliandika tena “Nategemea kuwajibishwa kwa watuhumiwa watakao patikana na hatia,sitegemei siasa tena hapo”

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa

Attachment