‘Msitu mnene haukosi vibweka’ Madee.

‘Msitu mnene haukosi vibweka’ Madee.

Ya nini tuutukuze uongo ilihali tu tuchekeane kiunafiki? Ni wazi hapa ni mahala pakusema ukweli wakati wote bila kujali nani ni nani.

Ingawa kwenye uhalisia “Ukweli unauma” lakini msisahau pia ukweli ni dawa. Kwa ukubwa wa msanii Madee hatuwezi kuacha kusema ukweli juu yake katika kazi yake ya muziki.

Wakati naona posti katika mitandao ya kijamii juu ya wimbo wake mpya wa hela, hakika niliona ni kazi kubwa, na niliona ni kubwa kwa kuwa tuliandaliwa hivyo kwa namna ya posti zilivyokuwa zinapostiwa na wadau pamoja na wasanii wengine.

Leo wimbo wa hela umetoka ambapo tumeona Madee akijaribu kufanya Rap ambayo aliwahi kufanya miaka kadhaa nyuma, ambayo alisema haiuzi. Sasa sijui hii itauza?

Ama kweli! “msitu mnene haukosei vibweka” maana Madee amafanya ule muziki ambao kwa muda mrefu yeye na uongozi wake wanaamini sio biashara. Lakini kibweka kingine ni jinsi ambavyo amerap ni kama msanii mchanga ambaye hajawahi kuingia studio.

Ila wimbo huu umefanyika Mj Record chini ya Daxchol na Marko Chal sasa nashindwa kuelewa kwanini hawakuona kama wimbo haupo sawa kwa Madee? lakini huenda ikawa muhusika ametaka iwe hivi iliivyo.

Ila ni ukweli mdundo uko sawa na Madee ameshindwa kabisa kuutendea haki.

Ni wazi wimbo huu haupo katika kasi ya ushindani kwasasa. Ila haitashangaza kungia katika chat mbalimbali za vituo kadhaa vya habari maana vingi havizingatii ubora wa kazi bali kujuana juana kusipo na maana wala tija kwenye maendeleo ya muziki huu wa kizazi kipya.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa

Attachment