‘Msinitenge’ ya Prof Jay ni aina ya tungo zilizokosekana kwenye muziki wa kizazi kipya sasa.

‘Msinitenge’ ya Prof Jay ni aina ya tungo zilizokosekana kwenye muziki wa kizazi kipya sasa.

Kila mtangazaji, mchambuzi, na hata bloggers ni watu wa kusifu nyimbo za starehe zaidi, na huku wakiaminisha wasanii kuwa muziki wenye mafundisho hauuzi kabisa.

Hoja hiyo wasanii wameichukua kama ilivyo, na wamekuwa wasanii wazuri katika kusifu pombe na ngono. Nafikiri ndio maana ya Afande Sele kusema katika wimbo wa Darubini Kali mwaka 2004 “Mnasifu pombe na ngono pumbavu hamna soni” Ni wazi wasanii wanasahau kuwa muziki licha ya kutoa uburudishaji pia muziki ni sehemu kubwa ya watu kupata mafundisho.

Msinitenge ni wimbo wa Pro Jay ambaye sasa ni Mh Mbunge wa Jimbo la Mikumi Mkoani Morogoro. Wimbo huo alimshirkisha Q Chillah na ni wimbo uliokuwa unapatikana katika album ya Mapinduzi Halisi iliyotoka mwaka 2003  ambayo ilitengenezwa na P Funk Majani ndani ya Bongo record.

Hakika wimbo huu unabaki kuwa bora wakati wote ambao ulieleza yote ambayo yalikuwa yanapotosha wengi juu ya  ugonjwa  wa Ukimwi. Prof Jay aliweza kutoa elimu kupitia muziki wake, na hakika wimbo huu ni moja kati ya nyimbo pendwa wakati wote hata kwa wale ambao sio mashabiki halisi wa muziki wa kizazi kipya.

Lakini katika miaka ya nyuma zipo nyimbo ambazo zilitoka zikiwa na tungo za aina hii, ambazo zimebaki kama alama katika muziki huu wa kizazi kipya. Wimbo kama Mshikaji mmoja wa Joslin, aka mimi ya Albert Mangwear, Kazeze ya OCG, Alikufa kwa ngoma ya Mwana Fa, Kosa la Marehemu ya Uswahilini Matola, Tutamtambuaje ya Wagosi wa kaya, Kama nitapata Ukimwi ya Afande sele, Mechi kali ya Solid Ground Family na Sukari ina pilipili ya Solo Thang.

Hizi zinabaki kama kielelezo juu ya nyimbo ambazo zilizungumzia swala zima juu ya maambukizi ya Ukimwi na jinsi ya kuepukana na maambukizi, lakini pia jinsi ya kuishi na waathirika,na hata kuwambusha watu kuwa sio kila muathirika amefanya ngono.

Amka msanii hakuna muziki usiokuwa biashara hivyo tunga tungo zenye kuelimisha jamii pia.

 

 

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa

Attachment