Msimu wa tano wa Coke Studio Afrika umeanza kwa burudani ya aina yake

Msimu wa tano wa Coke Studio Afrika umeanza kwa burudani ya aina yake, Msimu ambao umepewa jina la DISCOVERY (Gundua). Coke Studio Afrika ni jukwaa ambalo linawakutanisha wasanii mbali mbali kutoka katika nchi tofauti za Afrika pamoja na wasanii wakimataifa kutoka nje ya mipaka ya Afrika.

Mwaka huu Coke Studio Afrika imerudi kwa kishindo kingine kikubwa sambamba na theme ya mwaka huu ambayo ni DISCOVER, theme ambayo inaendelea kuijaza mioyo ya mashabiki na wapenzi wa muziki hamu ya kutaka kugundua nini hasa kimeandaliwa katika msimu huu mpya na watano.

Kama ulipata fursa ya kutazama show nzima ya Coke Studio Afrika Jumamosi ya tarehe 10, Spetemba, hakika hautajutia kutumia muda wako kuitazama. Msimu wa tano umefunguliwa na show kali kutoka kwa Ray Vanny akiwa moja wapo ya wasanii wanaiwakilisha Tanzania katika msimu huu.
Katika kipengele cha Cover, Ray Vanny ameimba ‘Imperfeito’, wimbo wa Dji Tafhina, msanii kutoka Angola. Wakati Dji Tafhina akiimba ‘Natafuta Kiki’ ya Ray Vanny.

Kipengele kilichofuata ni Throwback mbacho ambapo Bebe Cool msanii kutoka Uganda alishirikiana na Falz mkali kutoka Nigeria ambao kwa pamoja waliimba ‘Boju Boju’.

Hakika msimu huu umeanza kwa style ya aina yake, kama wasemavyo wahenga, “Yanini tuandikie mate na wino ungalipo” Kama ulikosha kutazama kwenye TV nafasi bado unayo. Bonyeza play kutazama Coke Studio Season 5 Episode 1.