Msanii wa Kenya afanya cover ya ndindindi ya Lady Jaydee

JAY-DEE-620x360

Ndindindi ni wimbo unaofanya vyema katika vituo vya radio na runinga ndani na nje ya nchi, wimbo huu ni wimbo halali wa mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Lady Jaydee ambaye ni wazi ameendelea kuwa bora kila siku tangu kufahamika kwake kimuziki.
Katika hali ya kuonekana kuwa ujio wake huu umekuwa bora zaidi ni pale msanii kutoka Kenya Wangechi alipoamua kufanya cover ya wimbo huu wa ndindindi. Ambapo Lady Jaydee hakuweza kuficha furaha yake pale alipoamua kuweka post katika mtandao wa picha Instagram na kusema “Kenya Stand Up NdiNdiNdi Cover @wangechikenya #LoveFromKenya #NdiNdiNdi #NguvuYaUmma #WananchiWameipokea #MapenziKutokaKenya

Wangechi ni msanii wa hiphop anaefanya vyema sasa katika ramani ya muziki Kenya. Tazama chini video ya wimbo huo kutoka mtandao wa picha Instagram.
Picha ya msanii Wangechi
wangechi2


www.tizneez.com
Twitter tizneez
Facebook tizneez
Instagram tizneez
Youtube tizneez