MSANII MENEJA ANASTAHILI HESHIMA

kp15102014
Tanzania ni miongoni mwa nchi yenye wasanii wengi zaidi duniani na kadri siku zinavozidi ndio idadi inakua kubwa tunaona mafanikio yasiyojificha hasa katika tuzo mbali mbali zinazofanyika ndani ya Afrika na nje ya Afrika.

Kama tunavo amini kila kazi ikiwa na usimamizi mzuri itafanikiwa kwa kiasi kikubwa haijarishi ni kwenye ngazi ipi au kitengo gani na vivyo hivyo hata msanii nae anapaswa kuwa na usimamizi wa kazi zake ili kuweza kupata mafanikio kwa urahisi zaidi na kuweza kufika mbali.

Nikizungumzia ma meneja wanao wasimamia wasanii hapa tanzania najua majina haya lazima yatakua akilini mwako ambayo ni Said fela,babu tale,mubenga, na Ostadh juma na musoma hawa ni baadhi yao na kila mmoja anafahamu mchango wao katika muziki na maisha ya wasanii mpaka sasa.

Kwa kudhihilisha kuwa msanii anahitaji usimamizi ili aweze kudumu na kuendelea kuwa ni bidhaa nzuri katika tasnia ya muziki ni lazma apate usimamizi makini na wenye mtazamo wa mafanikio katika pande zote mbili.

Hawa ni baadhi ya wasanii ambao walifanya vizuri wakiwa ndani ya usimamizi na walivo ondoka tu basi ubora wao ulishuka sana na kuonekana kama ndio wanaanza mziki na wengine kupotea kabisa mfano

HUSSEIN MACHOZI
Huyu ni msanii ambae alikua chini ya usimamizi wa Tetemesha Record chini ya KIDBWOY na aliweza kufanya vizuri na kuingia katika chat mbalimbali za radio ndani na nje ya Tanzania na alifanikiwa kufanya kazi na msanii wa kenya DNA katika hit ya Full shangwe mbali na hiyo pia anahit kibao zilizokuna vichwa vya mashabiki wake na wapenzi wa mziki kama vile Promise,kafia Gheto,utaipenda,kwaajiri yako na nyingine nyingi.lakini baada ya kuachana ya usimamizi huo alishuka kimuziki na ukilinganisha na sasa.

SPARK
Hakuna asie jua ubora wa spark katika uimbaji wake spark alikua akisimamiwa na babu tale katika familia ya Tip Top connection na kufanikiwa kufanya kazi kubwa ya Ripoti za mtaa akishirikiana na madee pamoja na tunda man nakuacha historia ambayo hata yeye leo anaikumbuka lakini spark yuko wapi leo spark ndio nani leo katika mziki wetu wa kizazi kipya.

SUMMA MNAZALETI
Huyu naweza kusema ni rapa mahili na mtunzi anaeweza kuteka hisia za mashabiki kwa kile anacho kiimba summa mnazaleti alikua ni msanii wa familia ya mtanashati chini ya ostadhi juma baada ya kutoka lunduno kipindi cha nyuma na alifanikiwa kuibeba kweli mtanashati na kuweza kufanya hit kama Asante na Chukua Time alio mshirikisha Ommy Dimpoz nafasi yake imetoweka kwa sasa na hiyo yote ni kutokana na kuondoka katka usimamizi uliokuwa unamsimamia.

SAJNA
Wimbo wa iveta ndio uliofanywa na sajna msanii kutoka mwanza ambae alivuma na kutabiliwa makubwa sana katika kiwanda cha muziki wa kizazi kipya tanzania sajina alikua Tetemesha Record chini ya Mtangazaji wa RFA KIDBWOY lakini sajna hakufika pale alipo tarajiwa na watu wengi baada ya kuachana na KIDBWOY ambae ndie alikua mtambuzi wa kipaji chake.

Wapo wengi sana lakini hawa ni mifano tu ya baadhi ya wasanii ambao walifeli kwa kutokuelewana na usimamizi wao japo kila upande unamapungufu yake lakini tunapaswa kuvumiliana ili tuweze kutimiza malengo malengo yetu kwa usawa na haki.

Makala hii imeandikwa na John unaweza kuwasiliana nae johndamsony@gmail.com 0788 584 910