MSAGA SUMU ASHANGAZWA KUZUSHIWA KIFO

IMG_3229
Msaga sumu ni msanii anaefanya vizuri katika mziki wa uswahilini almaarufu kama kisingeri,Msaga ambae kwasasa ameonekana kuwa kipenzi kwa watanzania waliowengi kupitia aina ya muziki anaofanya.
Licha ya kufanya mziki ambao hauchezwi mara nyingi kwnye vituo vya radio lakini Msaga Sumu amepata nafasi ya kutunga wimbo unaotumika katika kampeni za urais kupitia chama cha Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa.
Baada ya taarifa kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii na pia kwenye baadhi ya magroup ya watsap,juu ya taarifa za kifo chake ambacho ilisemekana amefariki kwa kupigwa risasi.Team tizneez ilitamfuta mtu wa karibu wa Msaga Sumu ambaye hakutaka jina lake litambulike ambapo alisema”Msaga yuko poa anafanya shughuli zake.
Tema tizneez haikuishia hapo iliamua kumtafuta Msaga Sumu.Akiongea kwa njia ya simu ya Msaga Sumu alisema “aiseha nashangazwa na uvumu unaoendelea na hata sijui ni nani anatoa taarifa hizi,lakini nataka watu wajue nipo fresh nafanya kazi zangu na muda huu nipo nyumbani kwangu.Watu waachane na hizi longolongo zisizo na maana kiukweli nashangazwa na huu uvumi.Nipo salama na sijapata tatizo lolote.”Alisema.
Mwisho
Piga kura linda amani.#tiznnez.com
Facebook.com/tizniz

Twitter.com/tizneez

Instagram/ tizneez