“Mrisho Mpoto ulistahili kukatwa nywele na kupigwa risasi tano hadharani” Afande Sele.

“Mrisho Mpoto ulistahili kukatwa nywele na kupigwa risasi tano hadharani” Afande Sele.

Afande Sele ni msanii wa hiphop ambaye nyakati zote amekuwa na misimamo yake tofauti na wasanii wengi. Na nyakati zote hutoa mitazamo ambayo ni wazi wengi hushangazwa kwa namna ya utojai wake mitazamo.

Mapema leo kupitia mtandao wa picha Instagram Afande Sele ametoa mtazamo wake juu ya wimbo wa uzalendo ambao umekusanya wasanii wengi, lakini Mrisho Mpoto akionekana ni kinara wa kukusanya wasanii hao.

Afande Sele ameandika “Rafiki yangu mkubwa mjomba mpoto kama ni kweli wewe ndio ulikua kinara katika kusimamia utayarishaji wa wimbo maalumu wa kuhamasisha uzalendo kwa taifa halafu ukashawishi kuondolewa kwa baadhi ya wasanii wazawa ndani ya wimbo huo na badala yake ukampa nafasi rafiki yetu Christian Bella.

Kushiriki katika wimbo huo unaowahusu watanzania wakati ukijua wazi kuwa Bella pamoja na ukweli ni rafiki yetu sana lakini bado yeye sio mtz bali ni mcongoman.

Katika hili mjomba umetukosea sana watanzania wenzako na kwa hakika kama ingekua kitendo chako hicho umekifanya kwa nchi zilizoshiba uzalendo na zisizovaa joho la unafiki mjomba ulistahili kukatwa nywele zako na kupigwa risasi angalau tano kichwani kwa uchache tena hadharani kwani ulichofanya ni usaliti kwa nchi yako na ni aina flani ya uhaini…

 

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa