MR II SUGU AWEKA KUMBUKUMBU ZAKE MTANDAONI

IMG_2841

MR II SUGU AWEKA KUMBUKUMBU ZAKE MTANDAONI

Joseph Mbilinyi ambaye ni maarufu kwa jina Mr II Sugu ambaye sasa ni Mh Mbunge wa Mbeya Mjini, pia ni mbunge aliyeshinda kwa kuchaguliwa kwa kura nyingi kuliko mbunge yoyote katika uchaguzi mkuu October 2015. Sugu alishinda ubunge kwa mara ya kwanza mwaka 2010.

Sugu ni moja kati ya wasanii wachache waliochonga njia ya muziki wa kizazi kipya, ambapo licha ya kuchonga njia ila ni miongoni mwa wasanii wachache tena waliojitoa kupigania muziki katika kupata haki mbalimbali ikiwemo ya haki miliki na hata malipo ya mirabaha.

Licha ya kuwa Mbunge lakini ameendela kuonyesha safari yake maisha hata katika kitabu chake cha Autography ameeleza mengi yenye kumtia moyo kijana ambaye yuko mtaani akiwa na ndoto nyingi, ambapo katika itabu chake ameandika “ ni juhudi pekee zinazoweza kumfikisha mtu popote atakapo.”

Kupitia mtandao wa picha Instagram Sugu aliweka ukumbusho wake ambapo alisema “I know about life…Hizi ni gloves halisi nilizowahi kutumia wakati flani ‘nilipolazimika’ kufanya kazi US Post katika mihangaiko ya maisha Ughaibuni, na mpaka leo nimezitunza kama kumbukumbu ya machungu.. So pliz be careful when u wish for my down fall… Coz u probably don’t know me!!…I’m a nigga who always turn my weaknesses to be my strength!! N I never loose, I either win or learn”

Tazama chini picha hiyo.Post yake Mr II sugu

SUGU

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez