Mr Blue Amshushia tuhuma Mr II Sugu

mrblue
Mr Blue Amshushia tuhuma Mr II Sugu
Sintofahamu imeibuka kwa mashabiki wa Sugu baada Mr blue kuweka post katika mitandao ya kijamii ambayo ni wazi ametoa shutuma juu Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu.
Mapema leo Mr Blue ameandika katika mtandao wa picha Instagram ambapo ameandika”Ndugu zangu nipeni ushauri kwa hili niliona nikae kimya ila limeniuma sana kwa kweli SUGU namuheshimu kama kaka yangu kimuziki na kiumri pia. Sasa kuna nyimbo nilimshirikisha inaitwa “Freedom” tulifanya pale kwa makochali na hiyo ndo picha ya ushahidi na nyimbo ipo youtube kwa wasioisikia..sasa kinachonishangaza leo kuona ameitoa verse yangu na kuweka verse zake mbili na kaishoot mpaka video na nyimbo imekuwa yake tena bila kunitaarifu mimi mwenyewe au ridhaa yoyote kutoka kwangu je hii ni haki kweli??? Maana mtu ukiongea unaonekana unatafuta kiki au sijui nn…mi imeniuma kwa kweli jamani je mnanishauri nini ndugu zangu.”
Team tizneez inaendelea kumtafuta Sugu ili kuthibitisha hili.

www.tizneez.com
Twitter tizneez
Facebook tizneez
Instagram tizneez
Youtube tizneez