Moni Centrezone agongwa na gari.

Moni Centrezone agongwa na gari.

Moni ni msanii mbaye anaunda kundi la Moco akiwa na Country Boy.

Ambapo amepata ajali ya kugongwa na gari maeneo ya Sinza La Chalz Pub, Alfajiri ya leo walipokwenda kununua chakula akiwa na msanii mwenzake Country Boy.

Counrty Boy akiongea kwa njia ya simu na Team Tizneez ameeleza “Moni amepata ajali Sinza, na jamaa amemgonga aliporudisha gari kwa nyuma.

Na chanzo ni jamaa kutugonga sisi na gari yetu alipokuwa anagombana na wenzake, sasa tunashuka tu kwenye gari yetu, jamaa akarudi nyuma tena kwa kasi ule upande wa Moni ndipo alipoweza kumgonga kwenye mguu wake.

Na mpaka muda huu Moni anaendelea vizuri hivyo tunamshukuru Mungu maana hajapata matatizo makubwa.

 

Picha chini Moni akiwa hospital.

Team Tizneez tunatoa pole kwa Moni Centrezone, na apone haraka aweze kuendelea na majukumu yake.

#TuzungumzeMuziki