Mke wa Roma athibitisha uwepo wa Roma katika mtandao wa picha.

Mke wa Roma athibitisha uwepo wa Roma katika mtandao wa picha.

Roma ni msanii wa hiphop ambaye amejipatia umaarufu wake kupitia tungo zake zilizobeba ujumbe wa maisha ya watanzania walio wengi.

Tanzania ni wimbo wake wa kwanza uliomtambulisha vyema katika ramani ya muziki wa kizazi kipya mwaka 2007.

Mwaka huu 2017 katika miezi michache iliyopita Roma na wenzake walipata matatizo ya kutekwa na watu wasiojulikana. Ambapo baada ya siku kadhaa walipatikana wakiwa ni watu wenye majeraha mbalimbali.

Tangu kupatikana kwa Roma hakuwa anaonekana katika mtandao wa picha kama ambavyo ilikuwa ni kawaida. Na kumeibuka kurasa nyingi ambazo zina mfanano wa jina lake alilolokuwa anatumia “Roma2030”.

Mapema leo kupitia mtandao wa picha katika posti ambayo aliweka msanii Dayna Nyange ambayo katika posti hiyo aliweka picha akiwa na Roma, na wakati huo akiwa ameonyesha ukurasa wa Roma2030.

Mke wa Roma ambaye ni maarufu kwa jina la Mrs Roma katika mtandao huo wa picha alikomenti kwa kusema “Futa hiyo tag iyo account unampa promo mtu tofauti”

Lakini pia Mrs Roma aliendelea kumjibu shabiki ambaye alimuelekeza  Dayna Nyange namna ya kuandika jina la Roma ambalo anatumia katika mtandao huo wa picha. Ambapo mke wa Roma ajibu kwa kuandika “ Kwa kifupi Roma kwasasa hana account insta hata hiyo sio yake bro”

Hivyo mashabiki wa Roma ni wazi kwasasa msanii huyu hana ukurasa wa mtandao wa picha.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa