Misimamo ya Nash Mc yatua kwenye chuo kikuu Ujerumani.

Misimamo ya Nash Mc yatua kwenye chuo kikuu Ujerumani.

Nash ni moja ya wasanii wa hiphop ambao wakati wote amekuwa ni mwenye misimamo kwa kutetea maslahi yake na hiphop kwa ujumla.

Mapema leo kupitia mtandao wa picha Instagram ameandika

 

“TAARIFA:
Kwanza Kabisa Namshukuru Mwenyezi Mungu na familia yangu pamoja na taasisi yetu ya KINASA kwa kubariki Kila Mambo nalofanya. Kubwa kabisa ni kutaka kuwapa taarifa rasmi wapenzi,wafuasi na wakereketwa wote wanaokubali Harakati zangu popote walipo.

Napenda kuwajulisha Kua kwa sasa nipo nchini Ujerumani katika mji wa Bayreuth, nilifika jana jioni na leo nikasema niwajuze kilichonileta huku. Ndugu yenu nimealikwa katika Kongamano la Kiswahili katika chuo kikuu cha Bayreuth ambalo hufanyika Kila mwaka na hili ni Kongamano la 30 mwaka huu.

Lakini pia nimepata nafasi ya heshima ya kupiga onesho siku ya Jumamosi ambayo ndio itakua siku rasmi ya kusherehekea miaka 30 ya Kongamano hilo. Baada ya hapo nitashiriki katika mjadala wa mahusiano ya Lugha na Maarifa na hapo nitachambua kuhusu Utamaduni wa Hip Hop na ushirikiano wake na Lugha ya Kiswahili katika kuwapa watu maarifa.

Kwa kweli ni hatua kubwa za kimafanikio kwa watu wote wanaopenda maendeleo ya Kiswahili na Utamaduni wa Hip Hop halisi kwa ujumla na sio kwangu tu. Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunichagua katika kuwakilisha Tanzania na Utamaduni wangu wa Hip Hop Ulimwenguni.

Ujerumani ni moja kati ya nchi zinazothamini utamaduni wa Afrika lakini ndio nchi iliyo juu katika masuala ya Hip Hop kwa sasa duniani,Mejah Mbuya anafahamu hilo kwa kina jamaa wana ile Hip Hop yenyewe kabisa ambayo haijaingizwa ujinga.

Nategemea kuwepo hapa kwa Juma moja na baadae nitarejea Tanzania . Kuna mambo mengi ya Kuongea na nyie wafuasi wangu ambao mmekua mkitukanwa kutwa kucha kwamba Nash amewapa nini sijui hamumkosoi Nash na mambo kibao lakini haya ndio majibu yake.

Nash naamini nachokifanya na naamini rizki anatoa Mungu wala sio Radio au TV. Hip Hop nayohubiri inanipa mwanga na mafanikio lakini yote inachangiwa na uvumilivu na nidhamu kubwa niliyonayo katika kazi yangu.

Naungana na mswahili,mpambanaji mwenzangu Vitalis Maembe katika kuwakilisha Taifa. Tuwasiliana baadae kwa taarifa zaidi.”

 

 

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa