MINZI MIMS WASANII BONGO FLEVA/MUVI HAWAJITAMBUI

IMG_3583

Minzi Mims ni video director anaefanya vizuri kwa sasa ambaye amefanya video kama,Run dsm ya P the mc, Raha ya Tid ,pamoja na nyingine nyingi.
Kuelekea uchaguzi october 25 mwaka huu watu wengi  wameendelea kutoa maoni yao juu kile kinachoonekana wasanii kugawanyika na kuonekana zaidi katika majukwaa ya siasa.Kupitia ukurasa wake wa facebook director Minzi Mims ameandika”Wasanii wa bongo flava na bongo movie nadhubutu kusema, asilimia kubwa hamjielewi kabisa hamjui thamani yenu kama wasanii mnatumiwa kama condom na mwisho wenu ni katika kapu la takataka.
Baadae mnaanza eti harakati za kudai haki zenu hizo pesa mnazolipwa katika siasa hamtatumia katika kipindi cha miaka kumi, mtaendelea kuomba michango kwa wananchi katika matatizo yenu.

Siasa ni mchezo mchafu

IMG_3966

Director Minz katika picha akiwa anafanya video ya Pah one

Unaweza kuwa rafiki yetu facebook.com/tizniz

instagram.com/tizneez

twitter.com/tizneez