“Mimi nimeamua kufuata muziki” Rama Dee.

“Mimi nimeamua kufuata muziki” Rama Dee.

Kikao cha family ni wimbo wake Rama Dee ambao umemtambulisha vyema kwenye ramani ya muziki wa kizazi kipya.

Lakini Rama Dee amewahi kufanya vizuri na wimbo kama, Sara, Kuwa na Subira, Kama huwezi, Usihofie wachaga, Kipenda roho na nyingine nyingi.

Akiongea na Team Tizneez Rama Dee hakusita kuweka wazi hisia zake juu ya wasanii ambao mara zote wamekuwa ni watu wa kufanya matendo ya ‘kiki’.

Ambapo Rama Dee amesema “Tuangalie kati ya kiki au muziki, ukichanganya hivi vyote shabiki unamchanganya hajui nini afuate kwako kwa maana ya muziki au kiki.

Rama Dee ameongeza kwa kusema “Mimi nimechagua muziki, mtu anaona muziki wangu kwanza halafu baadaye anifahamu na mimi.

Lakini si lazima afahamu mambo yangu ya ndani yako vipi mke wangu, wanangu au rafiki zangu wako vipi.

Muziki ndiyo unaweza kumpa furaha au matumaini ya yeye kufika sehemu Fulani. Mimi sifikiri kama kiki ni sehemu ya kufanya muziki wangu uwe juu”.

Mwisho.