“Mimi ndiye nimefanya kazi ya Diamond na Neyo “ Shedy Clever

da1a4de59991d3e79888f0f598ab126d

“Mimi ndiye nimefanya kazi ya Diamond na Neyo “ Shedy Clever

Ni moja kati ya watayrishaji wa muziki ambae alifanya vyema miaka kadhaa nyuma, na baadae kuwa kimya kwa muda mrefu.

Akiongea na Team tizneez hakusita kusema “Watu kuona nimekaa kimya wanahisi kama nimeishiwa, ila nimefanya kazi nyingi mwaka jana na mwaka huu. Najua wapo ambao hawajui ila mimi ndiye nimefanya kazi ya Diamond na Neyo. Pia kuna kazi nyingine nyingi tu kama ya Matonya, Chegge, na Cassimu. Ila sijui zinatoka lini maana wasanii wenyewe ndio wenye mipango nazo.

Pia nimefanya kazi mpaka Afrika ya kusini na Nigeria. Hivyo watu wajue nipo na sijaishiwa.”

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez