“Mimi namuunga mkono Ruby” Sehemu ya 8-7

“Mimi namuunga mkono Ruby” Sehemu ya 10-9

:Part 8

Kweli rec lable ziliweza kusimamia kazi za sanaa na kuanza safari ya kubadilisha mziki kutoka kwenye mfumo wa BURUDANI hadi leo tunauita BIASHARA
Sasa baada ya mziki kuwa unaingiza chochote kitu wadau wakaona fursa nyingine ya ziada ya kutengeneza kipato cha hawa wasanii mbali na kuuza kanda yaani album wakabuni kufanya matamasha na wakapata idea ya TAMASHA LA FIESTA haswa lengo likiwa kwa kuwa radio station wanayo na wana rec lables zinazozalisha wasanii na wanapendwa pia wanauza kanda zenye nyimbo zaidi ya 5 wakaona sio mbaya wawakutanishe wasanii wanaofanya vyema sokoni na wananchi ambao ndio wanunuaji wa kazi hizo za sanaaa. Idea yao haikugonga mwamba ikafanikiwa kwa asilimia 100. Kama utakuwa namimi sambamba utaona makundi mawili moja TBC lililoshikilia mziki wa watu wazima na CLOUDS mziki wa kizazi kipya. Lakini si kuwa nawalaumu vituo vingine vya radio hapana pengine malengo ya kuanzishwa kwa vituo vyao haikuwa kama ya clouds maana clouds kauli mbiu yao ni BURUDANI JADI YETU. Na mifano ya kukuthibitishia hilo kwa miaka yote smooth vibe ndio ilikuwa ikishikilia na ndio ilizalisha wasanii asilimi 75 ya waliokuwa wakifanya vyema na sidhani kama yupo wakupinga juu ya harakati za clouds fm kuibua vipaji tangu huu mziki uanze mpaka miaka ya 2000 msanii naemjua ambae alifanya vizuri nje ya clouds fm ni 20% ambae alikuwa akipewa sapot ya asilimia mia na kituo cha magic fm, kama yupo mwingine utanisaidia yawezekana nimemsahau. Sasa hapa likaibuka tatizo jingine ambalo pia ni mzizi wa fitina yaaani kila unaemuona kwenye ramani ya mziki chimbuko la kujulikana kwake ni clouds fm. Hivyo hata wasanii wa mikoa.mbalimbali na wa dar waliokuwa wakichipukia walikuwa wakiamini ili wafikie malengo yao kimziki waende clouds fm. Maswali ya kujiuliza kwa nini radios nyingine hawakuwa wakizalisha wasanii??? Nini sababu iliopelekea kwa zaidi ya miaka 10 kuwa na tamasha moja tu kila mwaka linaloandaliwa na clouds??? Ukikaaa ukijiuliza kwa kina utagundua clouds wakawa wenyewe kwenye dunia yao.
Part 7
Mziki ukawa umepamba moto kuhusu matamsha yaani kipato ambacho kilikuwa tegemezi kikahama kutoka kwenye album hadi matamasha na kuwaaminisha wasanii kuwa waweza kutoa wimbo mmoja ukakunufaksha kwa matamasha mbalimbali kuliko kusubiri kugonga copy kwa muhindi na wasanii kwa kuwa wengi wao wanajua kuimba na sio biashara wakajikuta  wameamini sana kwenye matamasha na wimbo mkubwa uliofanya album zife ni MUM MWIZI na jina walilokuwa wakimuita mdau huyo mkongwe wa kuuza kazi za sanaa mwenye asili ya kihindi walimuita MDOSI. Basi kweli album zikakata na ikawa inawezekana kabisa ukaishi kwa single na matamasha yakaendesha maisha yao bila kuelewa kuwa mziki unakuwa kama gharama ya chochote kilichotengenezewa mfumo zamani kingekuwa kikipanda hivyo album ingekuja kuwa na gharama kubwa tu kutokana na hali ya soko kama tungeiundia mipango thabiti. Sasa hapa wasanii wengi waliokuwa wakifanya kazi nzuri wakawa ni wapya na sio wakongwe walioko kwemye nafasi za juu hivyo ki biashara lazima uangalie cost na faida hivyo automatic wadau wakawekeza nguvu kubwa kwenye new smooth vibe walioipa jina la T.H.T Tanzania House of Talent jumba la vipaji ambapo kazi yao ikawa ile ile ya kuibua vipaji na ukiangalia wengi leo wanaoendesha maisha yao walipitia au walitokea THT.

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez