“Mimi namuunga mkono Ruby” Sehemu 6-5

“Mimi namuunga mkono Ruby” Sehemu 6-5

“Mimi namuunga mkono Ruby” Sehemu 10-9

“Mimi namuunga mkono Ruby” Sehemu 8-7

Part 6
Mfumo ndio tatizo kubwa maana kwanza wasanii wamekuwa wengi kuliko wadau na hili bomu tulilitengeneza wenyewe wasanii wote kuielemea taasisi moja tukishirikiana na taasisi nyingine zilizokuwa zikiweza kuyafanya haya mapema na kujikuta sasa hiv wanakumbuka shuka kumekucha… waswahili husema ujana wako ule na nani uzee wako uniletee mie. Wasanii wamekuwa wengi mno hivyo mdau ni haki yake kuangalia nani anaemfaa kibiashara ambapo atapata faida na sio hasara kwa kuwa ni soko huria kwa maana yawezekana akakualika ufanye tamasha lake kwa mil 1 ukakataa lakini yupo kama wewe ambae haitaji chochote hadi usafiri anajigharamia nia yake anaihitaji platform ya kulitumia jukwaa la tamasha husika kujitengenezea ugali wa mbeleni.

Mimi wakati ni mfanya kazi wa clouds nilimshuhudia diamond platnum akipanda jukwaa la fiesta kwa mara ya kwanza na steg show wasiopungua 5 wakiwa wamependeza mnooooo na wamejigharamia kila kitu na walijitolea yaani diamond hakulipwa na walitambulishwa ye na jux kama sikosei nafikiri wote leo ni wasanii wenye mafanikio makubwa saana ila sasa jiulize swali kama mdau anakulazimisha mbona diamond hapigi show za fiesta na nyimbo zake zinachezwa!

Kama kweli wadau usipokubali show zake ndio anakuuwa kisanii wai diamond stil there ni maswali ya msingi ya kujiuliza kabla ya kuendelea kulalamika kwa mkumbo. Wasanii ni kujitengeneza na kujua thamani yako na ikiwezekana utapogundua madhaifu yako juu ya biashara weka watu wakusaidie ambao wanaijua biashara kuliko wewe ili utengeneze pesa.
Part 5
Sasa wapi wasanii tunakosea sisi kwa sisi ni maadui wakubwa. Hatupendi mwenzetu afanikiwe na tumekuwa tukiombeana anguko la wenzetu kila kukicha hatuna UMOJA. Mwanzo wa mwaka huu serikali yetu imetangaza kuwa kila radio na tv ikicheza kazi ya msanii inatakiwa ilipe kama inaingiza pesa kutoka kwenye matangazo na ni sheria hiyo imepitaa haina msalie mtume ni kama sheria nyingine zinazotekelezwa na ukikiuka yakupasa uchukuliwe hatua lakini hadi leo ni nani anaongelea MRABAHA yaani pesa zitokanazo na malipo ya matangazo.

Tulitumika sisi kupaza sauti kusema ya kuwa hatutaki kulipwa ona kazi ngumu tuliyowapa COSOTA kushindwa kuikusanya mirabaha kwa properganda za kuwa vyombo vya habari vinatozwa pesa nyingi. Sasa hapa ndipo pa kujifunza maana sisi wasanii kuna kundi wanasema wanataka kulipwa na kuna kundi linasema hatutaki kulipwa na haya makundi mawili yanavutana kweli hakuna anaetaka mwenzie ashinde ila hawa wamiliki wa vyombo vya habari ambao tunasema ni washindani wana mabifu hawaelewani wameunda umoja wao kutukabili.

Asa inachekesha kuona msanii analalamika huku maslahi hakuna na kwenda kwa mdau mwingine ambae wanawasiliana wamiliki kila kukicha ni mbinu gani watumie ili waendeshe maisha yao… kwanini hatujifunzi mfano mimi kuna kituo hakichezi wimbo wangu kwa kuwa nimekiuliza kwa nini wanawasainisha mikataba wasanii ili wacheze kazi zao bure hao hao watasema wanasimamia haki kuna kituo hakipigi tena kazi za man fongo kwa kuwa hakwenda kwenye show yao akaenda kwenye kituo kingine leo hii hao hao waliowahi kuumizwa wamesikia ruby kazingua kituo kingine hajaenda kwenye show wamemkumbatia kwa mikono 2 hiv jamani wasanii tumelogwa na nani? Kwani hatujui hawa wadau ni kama madreva boda boda au bajaji lao ni moja tu wafaidike?

itaendelea…..

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube Tizneez