Mh.JOSEPH MBILINYI “SUGU”NAWAKALIBISHA WANAOTAKA MABADILIKO

IMG_2803

Mbunge wa Mbeya Mh Joseph Mbilinyi maarufu kama Mr II Sugu,ambae ni msanii wa muziki wa hip hop na mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chadema.Pia ni msanii wa hip hop anaeongoza kwa kuwa na album nyingi,ambapo mpaka sasa amefikisha album kumi na moja(11) album hizo ni Ni mimi ambayo ilitoka mwaka 1995,Ndani ya bongo 1996,Niite Mister II 1998,Millenium 2000,Muziki na maisha 2001,Itikadi 2002,Sugu 2004,Coming of age ujio wa umri 2006,Veto 2009,na Ant virus mixtape.

Katika tamasha la Democracy in dar lilifanyika jana  katika viwanja vya Zakhem Mbagara  Mh Joseph Mbilinyi akiongea na Team tiznez alisema “Huu ni muunganiko wa wasanii wanapenda mabadiliko na bila kujali nani ni nani hivyo napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha wasanii wengine katika hili swala la kutaka mabadiliko,na kuelimisha zaidi vijana wenzetu katika swala zima la upigaji wa kura.

Mh Joseph Mbilinyi pia lishiriki kikamilifu katika kutoa burudani katika tamasha hilo la democracy in dar akiwa na mmoja kati ya wanaunda kundi la Wagosi wa kaya Mkoloni na kushangiliwa na mashabiki wake walionyesha kuwa wanamuhitaji pia katika muziki.

Mwisho.

Unaweza kuwa rafiki yetu faceboo.com/tizniz

instagram.com/tizneez

twitter.com/teamtizneez