Mgosi Mkoloni Amtaka Mh Paul Makonda kuanza na yeye.

IMG_2815

Mgosi Mkoloni Amtaka Mh Paul Makonda kuanza na yeye.

Kupitia mtandao wa Facebook msanii na mkongwe wa muziki wa kizazi kipya na Mwenyekiti wa TUMA ndugu Fredrick Malick maarufu kama Mgosi Mkoloni.

Kupitia kile kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kauli ya Mh Paul Makonda ambapo inadaiwa amesema “Utafanyika msako wa nyumba kwa nyumba kwa wakazi wa Dar es salaam ili kubaini wale wasiokuwa na kazi maalum” Lakini katika mitandao ya kijamii wengi wameandika kuwa “Mh paul Makonda amesema atawakamata wale wasio na kazi watakamatwa na wale watakao kwamisha zoezi hilo”

Kupitia kauli hizo msanii na mwanaharakati wa mambo mengi amefungua mdomo wake na kuandika kwenye mtandao wa kijamii Facebook. Ambapo ameandika

“Sina kazi yoyote na mzururaji tu massa 24 na ninaishi Karakata nyumba namba 76……..njooni muanze na mimi mapema asubuhi na napatikana vijiwe vyote kuanzia baracuda,bondeni,kisimani,relini na njia panda ya airport…….kuongezea tu tupo kama washkaji 15 hatuna kazi tunazurura tena kwa uhuru na hatuna kazi yoyote anzeni na sisi! Naongea mimi hapa wala sipingi chenga…..kituko cha mwaka hiki”

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez