MFAHAMU GIHCUE DIRECTOR WA BURGER MOVIE SELFIE YA BELLE 9

0de0378
Gihcue pengine inaweza kuwa jina jipya kwa baadhi ya mashabiki wa muziki hapa Tanzania,Lakini si jina jipya sana kwa wengine waliona jina hilo katika video mpya ya Belle 9,Burger movies selfie.
Gihcue ni kijana toka Moro town,ambaye ameanza kufanya kazi ya muziki tangu 2008 mkoani Morogoro.Digital vibes ndio studio kubwa kwasasa mjini Moro town,inayoongozwa na mkali Gihcue.Ambao Digital vibes wamewahi kufanya wimbo wa Afande sele Dini tumeletewa,Nasisaka ya Chris wamarya,Kizungumkuti ya Mc koba,pamoja na ngoma nyingine zilizoko kwenye mixtape ya Country Boy.licha ya Gihcue kuwa mtayarishaji wa muziki Digital vibes pia jamaa anao uwezo mkubwa wa kufanya video.Na hili amethibitisha katika video mpya Belle 9
Burger movies selfie ni video ya pili ya mkali Belle 9 kuchezwa katika vituo mbalimbali vya tv hasa Trace music.Video hii imefanyika mkoani Morogoro na director Gihcue.
“Directors wa bongo wanajua kufanya video kali ili kinachowapeleka wasanii wengi huko nje ya nchi kuonekana tu nae kafanya kazi nje ya nchi.”Adili chapakazi
Hili ameonyesha Gihcue ambaye amefanya kazi ya msanii Belle 9 na kukubaliwa katika vituo vikubwa vya tv.Gih cue pia amewahi kufanya video ya tunavuka mipaka ya Team recers,No say by Kacci feat country boy,Team Racerz – Tell A Friend,TEAM RACERZ (TRLG) tunavuka mipaka,Jaggar Ft Ze Nova BIRTHDAY,na nyingine nyingi.Unaweza kucheki kazi zake nyingi kupitia account yake youtube “GIHCUE”
Team tizneez inakupongeza kwa kufanya kazi nzuri na kuonekana na walio wengi.
twitter@tizneez
instagram@tizneez