‘Merry You’ ya Diamond Platnumz feat Neyo imekopiwa kutoka kwenye wimbo wa Kcee Nigeria

‘Merry You’ ya Diamond Platnumz feat Neyo imekopiwa kutoka kwenye wimbo wa Kcee Nigeria

‘Merry You’ ya Diamond Platnumz Feat Neyo ni moja kati ya hatua kubwa ambazo Diamond ameendeea kupiga, na sisi yeye pekee bali katika muziki wa kizazi kipya kwa ujumla wake.

Hatuachi kusifu juhudi za Diamond ambazo kila leo amekuwa akifanya ili kufikisha muziki wa kizazi kipya duniani.

Imani ya wimbo huu wa merry you kuwa utamfikisha mbali zaidi ni kubwa mno, ilihali kumeingia dosari sasa juu kuwepo kwa wimbo wa ambao unaonyesha mfanano kwa kiasi kikubwa.

Mfanano huo umetoka katika wimbo wa Kcee ambaye ni msanii wa Nigeria,na wimbo huo unaitwa Fine Face ulitoka rasmi 2014.

Ingawa katika hoja ya kukopi wimbo ni hoja pana, yaweza kuwa makosa ya msanii au makosa ya mtayarishaji. Pia yaweza kuwa ni makosa ya wote wawili.

Lakini mashabiki wanapaswa kujua upo uwezekano wa wasanii kukubaliana katika kutumia mdundo, melody au hata kurudia wimbo wote kwa namna awezavyo.

Hivyo mpaka sasa bado haijulikani kuwa Diamond alizungumza na mhusika kutumia mdundo huo pia kutumia melody. Au ni ulikuwa ni uvivu wa kufikiri?

Sikiliza hapa chini wimbo ambao unaitwa Fine Face ambao inaaminika Diamond Platnmuz amekopi melody na mdundo.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa