Meneja wa Diamond Platnumz abanwa mahakamani

babu

Meneja wa Diamond Platnumz abanwa mahakamani.

Hamisi Shaban Taletale, maarufu kama Babu tale.

Kwa ufupi.

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupia pingamizi la Mkurugenzi wa Kampuni ya TipTop Connection ya Jijini Dar es salaam, Hamisi Shabani Taletale, maarufu Babu Tale, na kumtaka ajilezeni kwa nini asifungwe jela baada ya kushindwa kulipa fidia ya sh250 milioni.

‘Uamuzi huo umetolewa na Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Project Kayhyoza baada ya kutupilia mbali pingamizi la Babu Tale ambaye pia ni Meneja wa msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini. Abdul Nassib maarufu kama Diamond Platnumz.

Babu tale aliweka pingamizi kupitia jopo la mawakili wake wane, akipinga amri ya kukamatwa na kufikishwa mahakamani akidai taratibu za kisheria za kumkamata na kumfikisha mahakamani hazikufuatwa.

Alikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa amri ya mahakama, baada ya kushindwa kufika kusikiliza maombi ya utekelezaji wa hukumu ya mahakama hiyo iliyowamuru yeye na ndugu yake Iddi Shabani Taletale kulipa fidia ya sh250 milioni katika kesi ya ukiukaji hakimiliki.

Kesi hiyo ilifunguliwa na Mhadhiri  wa dini ya kiislamu Sheikh Hashimu Mbonde dhidi ya kampuni ya Tiptop Connection inayomilikiwa na ndugu hao baada ya kutumia mahubiri yake kibiashara bila ridhaa.

Mahakamana imetupilia mbali pingamizi hilo baada ya mmoja wa mawakili wake, Mugaya kutokufika mahakamani huku wengine waliokuwepo wakiomba usikilizwaji uahairishwe hadi tarehe nyingine. Baada ya kutupilia mbali pingamizi hilo,Msajili Kahyoza aliamuru bbau Taletale afike mahakamani Agosti 24 ili ajieleze ni kwanini asifungwe jela kutokana na kushindwa kutekeleza hukumu hiyo ya Mahakama.

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube Tizneez

Source Mwananchi