Mecky Kaloka Atoa ushauri kwa wasanii wanaofanya video nje ya nchi

227757_545907302087314_99215337_n

Mecky Kaloka Atoa ushauri kwa wasanii wanaofanya video nje ya nchi

Meky Kaloka ni moja kati ya waongozaji bora wa video hapa nchini Tanzania, mwaka 2014 alikuwa ni moja kati ya washiriki wa Tuzo za watu ambapo alikuwa akichuana na Nisher, na Adam Juma .Lakini Nisher ndiye aliyeibuka mshindi katika Tuzo hizo.

Akiongea na Team tizneez hakusita kuweka wazi juu ya wasanii walio wengi ambao wameonekana kufanya video nje ya nchi. Mekcy amesema “Mimi ninachoweza kuwashauri hawa wasanii ni kuto kuacha uhalisia wa kitu ambacho wanataka kutuonyesha. Watu wanaowaweka kwenye video, mazingira wanayotumia yawe yanaleta uhalisia na huku kwetu.

Kuna video nyingi hazina uhalisia, na umeona ni kiasi gani zinafungiwa. Ni wazi zimepoteza uhalisia ndiyo maana watu kama Basata na TCRA wamekuwa wakiingilia kati. Ila ni vyema tukafanya mambo yenye uhalisia zaidi.”

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez