MCHIZ MOX “AELEZA SABABU ZA WASANII WA ZAMANI KUTOFANYA VIZURI”

1375130295558

Mchiz Mox ni Hiphop star tokeo kundi la Wateule linaloundwa na Solo Thang, Jay Mo, Mchiz mox,na Jaffarah. Ambapo waliwahi kufanya vizuri na ngoma kama,Watu kibao,Msela,Bado yuko vilevile,pamoja na nyingine nyingi.

Mapema leo Team tizneez ilitamfuta Mchiz Mox ili kutaka kujua mtazamo wake juu ya wasanii wa zamani walio wengi kutofanya vizuri.Katika mahojiano hayo yaliyofanya kwa njia ya simu Mchiz Mox alisema “

Sidhani kama watu hawafanyI vizuri ila kuna baadhi ya watu wanafanya wasifanye vizuri, Unajua ushikaji kati ya baadhi ya wasanii na watu wa media ndo unasababisha yote haya.Unajua kuna wasanii flani na washikaji ambao wanaonana mara kwa mara so urafiki wao unaenda mpaka kwenye muziki yani kwenye kazi. Haimaanishi watu wasiwe washikaji ila kwenye kazi itazamwe kazi sio ushikaji.Watu wana experience ya kutosha kwenye huu muziki.Unajua sisi wasanii wengi wa zamani tumekuwa wakubwa so sio rahisi kuwa katika kumbi za starehe kila iitwapo leo,na huko katika makumbi ndo wanakuwa pamoja muda mwingi ndipo inapopelekea kuwa washikaji zaidi na baada ushikaji unahamia kwenye kazi. Na pia sisi nido watu tuliotengeneza foundation ya huu muziki mpaka leo unao una watu kibao, So tuheshimu ili tuendelee mbele zaidi ya hapa.”Alisema

www.tizneez.com

Instagram @tizneez

Twitter @tizneez

Facebook @tizneez