Mchiz Mox Aeleza sababu za wasanii kutoa rushwa.

1375130295558

Mchiz Mox Aeleza sababu za wasanii kutoa rushwa.

Watu kibao ni moja kati ya nyimbo zilizomtambulisha vyema katika ramani ya muziki wa kizazi kipya.

Watu kibao ni wimbo ambao ulitumika na bado unatumika katika simulizi moja nchini Ujerumani.

Akiongea na team tizneez Mchiz Mox hakusita kuweka wazi kile kinachofanya wasanii walio wengi kutoa rushwa zaidi katika vituo vya radio na runinga. Mchiz Mox amesema “ Wanatoa rushwa maana wasanii hawaamini katika vipaji vyao, hivyo inabidi watoe rushwa ili waweze kushawishi hao watu kupiga kazi zao. Mimi tangu nianze kufanya muziki sijawahi kutoa hela katika maisha yangu yote ya muziki. Ni zamani vipaji vilikuwa vinafanya kazi kuliko rushwa.

Mfano mimi nafanya hiphop na lazima ujue hiphop n muziki wa kueleza matatizo na ukombozi, sasa kama natoa rushwa nitakuwa nafundisha nini?

SOMA HAPA JINSI TEKNOLOJIA INAVYOPIGA TAFU MZIKI WETU

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez