MC KOBA “ZOEZI LA ZAWADI VIDEO LAKAMILIKA

12250189_10206845302564599_7668374537907463356_n
Msanii tokea moro town Mc Koba ambaye kwasasa anafanya vizuri na ngoma ya zawadi yenye mahadhi ya kiafrica zaidi iliyofanya na Mazuu recods.
Mc koba ambaye amewahi kuwa katika kundi la watu pori lililofanya vizuri miaka ya nyuma na baadae kujitoa katika kundi yeye na mwenzake Ditto na kufanya kazi zao na walibahatika kutengeza album moja.Album hiyo ilikuwa na wimbo pendwa zaidi ambayo iliitwa Ulibisha hodi,wimbo huu ulifanywa chini ya producer Majani ndani ya Bongo recods.
Zawadi ni wimbo wake mpya uliotoka katikati ya mwaka huu,licha ya kutanguliza audio pekee lakini sasa video yake ipo njian ambapo Mc koba alisema “Mungu mkubwa sana nimefanikiwa kumaliza zoezi la Zawadi video shooting, changamoto ni sehemu ya kazi nzuri siku zote. Kaa tayari kwa zawadi kwa mara nyingine tena.
Mwisho
Twitter@tizneez
instagram@tizneez