MATOKEO UCHAGUZI WA SHIRIKISHO LA MUZIKI TANZANIA (SHIMUTA)

IMG_6288

MATOKEO UCHAGUZI WA SHIRIKISHO LA MUZIKI TANZANIA  (SHIMUTA)

Shirikisho la muziki Tanzania (SHIMUTA)  limefanya uchaguzi katika kumbi za Basata zilizopo Ilala Dar es salaam. Shirikisho hilo ndilo litakalo simamia vyama vyote vya muziki vilivyo ndani ya Tanzania vinayotambuliwa na Basata.

Uchaguzi huo ulijumuisha nafasi ya Urais iliyokuwa inagombaniwa na Ado November na Samwel Mbwana ambaye katika kipengere hicho Ado November aliibuka kwa ushindi wa kura 14 na wakati mpinzani wake Samwel Mbwana kuibuka na kura 7, na kura hizi zilipigw ana wajumbe kutoka kwenye vyama mbalimbali vya muziki.

Pia katika uchaguzi huo ulijumuisha nafasi za ujumbe kwenye shirikisho hilo ambapo wajumbe walishinda ni Maumbile ally kura 7, Bakari Hasan kura 11, Kikute J Mpepo kura 15, Salim Mwinyi kura 11, Daniel Kamili kura 12, Daniel Laizer kura 15, pamoja na Samweli Mbwana kura 3.

Picha za uchaguzi katika kumbi za BASATA

IMG_6288

Picha!waliokuwa wanagombea nafasi ya urais walipokuwa wakisalimia kabla ya uchaguzi, kutoka kushoto Ado November ambaye ndiye aliyeshinda katika uchaguzi na kulia ni Samwel Mbwana.

IMG_6299

Wajumbe walipokuwa wakiwasiliza wagombea wakati wakiomba kura

IMG_6291

K wa mapacha akiendelea na kazi yake kama mwenyekiti  wa kamati ya uchaguzi ambaye amejizolea sifa kutoka kwa wajumbekwa kuwa mkweli na muwazi.

IMG_6326

Picha ya pamoja ya wajumbe na rais wa shirikisho la muziki tanzania

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez