Mashabiki wapuuzeni At na Peter Msechu.

IMG_2416

Mashabiki wapuuzeni At na Peter Msechu.

Leo hii ni siku ambayo wametangaza kutoa wimbo wao ambao wameshirikiana kwa pamoja.

Napata mashaka kwa njia ambayo walianza kutumia juu ya kutangaza ujio huo. Ambapo walikuwa wakiandikana kwenye mitandao ya kijamii katika hali isiyofaa yani hali ya ugomvi, kati ya At na Peter Msechu.

Shida ilikuwa juu ya mashabiki wao ambao nguvu kubwa waliitumia juu ya kumtetea msanii wake katika swala zima la maneno ambayo yalikuwa yanaendelea katika kurasa zao za mitandao yao kwenye mtandao wa picha “Instagram”

Lakini leo hii wapo pamoja na wanatoa wimbo wao, kwanini mashabiki wasiwapuuze? Maana nguvu waliotumia mashabiki katika kupinga hoja ya At na Peter Msechu katika hoja zao za kwenye kurasa zao za kijamii zilikuwa ni kubwa.

Hii inaonyesha ni jinsi gani hawakujali hisia za mashabiki wao, lakini kutoa wimbo ni mpaka utengeneze kiki za kipuuzi?

Muda umefika wa kuamka kifikra zaidi ni vyema kuheshimu mashabiki wako, kama unataka kutoa wimbo unaweza kutoa bila hata kufanya jambo la kipumbavu.

Siachi kusema kama wimbo ni mzuri basi utafanya vizuri tu, mfano ni wimbo wa sumu wa Fid Q wala haukuhitaji upuuzi wowote ili ufanye vyema bali muziki mzuri tu.

Mashabiki ni vyema kuwapuuza aina ya wasanii kama hawa ambao huwaona nyinyi mashabiki ni watu msio na akili.

Muziki bila kiki inawezekana.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez